Home » Jamii Ya Ogiek Yataka Serikali Kuharakisha Kuweka Mipaka

Jamii Ya Ogiek Yataka Serikali Kuharakisha Kuweka Mipaka

Jamii ya Ogiek/Picha kwa hisani

Jamii ya Ogiek sasa inataka Huduma ya Misitu ya Kenya KFS kuharakisha uwekaji mipaka wa msitu wa Mau ili kuepusha uvamizi wa wanyama eneo hilo.

 

Kupitia Mpango wa Maendeleo ya Watu wa Ogiek (O.P.D.P) jamii pia imeitaka serikali kuharakisha utekelezaji wa amri ya Arusha iliyotoa haki kwa jamii kupata sehemu ya msitu huo.

 

Jamii hiyo imesema ukulima haramu na malisho ya mifugo yanatishia sehemu za maji miaka miwili baada ya serikali kusitisha uangaziaji wa msitu wa umma katika kilele cha siasa za mohemko.

 

Goibei Sang akizungumza huko Mariashoni, Molo wakati wa ukumbusho wa sita wa uamuzi wa Mahakama ya Umoja wa Afrika mjini Arusha, Tanzania ametoa wito wa kuwepo kwa awamu mpya ya mashauriano ya pande mbili kati ya walengwa wa mpango wa ukodishaji na jamii ya Ogiek.

 

Haya yanajiri huku kukiwa na wito kwa serikali kuharakisha utekelezaji wa amri ya Arusha inayoruhusu jamii kupata sehemu ya msitu huo.

 

Mabishano hayo yaliibuka huku kukiwa na madai ya watu wengine katika mpango wa masharti ulioitwa mfumo wa Shamba, kukodisha sehemu za ardhi kutoka kwa Huduma ya Misitu ya Kenya ili kufanya kilimo cha misitu kwa gharama ya tamaduni za jamii.

 

Jamii ya Ogiek kwa pamoja inajumuisha wanachama 40,000 waliosambaa katika Kaunti za Narok, Nakuru, Kericho na Bomet.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!