Home » Koome, Jaji Lessit Wateuliwa Katika Kituo Cha Utafiti Wa Uhalifu

Koome, Jaji Lessit Wateuliwa Katika Kituo Cha Utafiti Wa Uhalifu

Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome na Jaji Jessie Lesiit wameteuliwa katika baraza kuu la Kituo cha Kitaifa cha Utafiti wa Uhalifu (NCRC).

 

Koome atawakilisha Polisi katika baraza hilo huku Lesiit akimwakilisha Jaji Mkuu.

 

Uteuzi wao umetangazwa kwenye notisi ya gazeti la serikali ya na mwenyekiti wa N.C.R.C na Mwanasheria Mkuu Justin Muturi.

 

Aidha Wataungana na Kenneth Odhiambo wa (Hazina), Jacinta Nyamosi wa kurugenzi ya mashta ya umma (DPP), Maurice Tsuma (Kamishna wa Huduma za Kijamii), John Warioba wa (Magereza) na Mary Mbau (Afisa Mkuu wa Marejeleo).

 

Wengine ni Judith Adongo, Samuel Ndiritu na Laureen Muisyo ambao wanaweza kuteuliwa na waziri kuwakilisha nyanja za sheria za uhalifu, sosholojia , uhalifu au kuwakilisha vyuo vikuu.

 

Katika notisi ya gazeti la serikali, Rais William Ruto ametangaza kuteuliwa kwa Ann Wambui Njuguna kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Uangalizi ya Uwezo Fund.

 

Wambui atahudumu kwa muda wa miaka mitatu kuanzia Mei 26, 2023.

 

Gavana wa Benki Kuu Patrick Njoroge pia ametangaza kubadilisha jina la First Community Bank Limited hadi Premier Bank Kenya Limited.

 

Mabadiliko ya jina yanakuja baada ya Premier Bank Limited ya Somalia kukamilisha ununuzi wa asilimia 62.5 wa First Community Bank.

 

Waziri wa Hazina ametangaza uteuzi wa Nicholas Kamuya Ng’arua kama mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji (CMA).

 

Kamuya atahudumu kwa muda wa miaka mitatu kuanzia Mei 26.

 

Ndung’u pia amewateua Hillary Marrimoi na Raymond Nyamweya kama wanachama wa Mahakama ya Ushindani kwa muda wa miaka mitatu kuanzia Mei 26.

 

Waziri huyo pia ametangaza kuwateua Tom Kimaru, Sammy Chepkwony, Caroline Bosco na Rosemary Wanjiru Thiongo kama wanachama wa Mahakama ya Bima kwa muda wa miaka mitatu kuanzia Mei 26.

 

Ndung’u pia ameteua Timothy Kimathi na Anthony Kiprono kama wanachama wa Mahakama ya Rufaa ya Mafao ya Kustaafu kwa muda wa miaka mitatu kuanzia Mei 26.

 

Waziri wa teknolojia na mawasiliano Eliud Owalo naye amebatilisha uteuzi wa David Mwangi Kuria na Ezekiel Onyango kama wanachama wa Baraza la Taasisi ya Mawasiliano ya Kenya.

 

Amewatoa Evalyn Koiyan na Bevin Angellah Bhoke badala yao. Watahudumu kwa muda wa miaka mitatu kuanzia Mei 26.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!