Home » Mahakama Yazuia Rais Ruto Kuagiza Mahindi Ya GMO

Mahakama Yazuia Rais Ruto Kuagiza Mahindi Ya GMO

Majaji watatu wametupilia mbali ombi la serikali la kutaka vyakula vya GMO kuruhusiwa nchini.

 

Majaji Mohammed Warsame, Ali Aroni na John Mativo wamesema kuwa ombi la serikali halina msingi na halijazingatia maslahi ya wananchi.

 

Kufuatia uamuzi huo, agizo la kuharamisha uagizaji wa vyakula vya kisaki litasalia hadi kesi iliyowasilishwa na wanaharakati wa Kenyan Peasants League, isikizwe na kuamuliwa.

 

Serikali ilikuwa ikidai kuwa vyakula vya GMOs vitasaidia kuhakikisha utoshelevu wa chakula nchini na kupunguza bei ya vyakula vya wanyama.

 

Katika uamuzi huo wa kurasa 21, Mahakama ya Rufa haikupata uhalali wowote katika kesi hiyo, ambayo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliitetea Serikali.

” Katika Chama cha Sheria cha Kenya dhidi ya Chama cha Wanablogu Kenya & Wengine 6 (2020) eKLR. Mwishowe, hatuoni umuhimu wowote katika ombi hilo kwani waombaji hawakuturidhisha kwa sehemu zote tatu,” ilisoma sehemu ya uamuzi huo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!