Home » Polisi Wawatawanya Wafuasi Wa Maina Njenga

Maafisa wa Polisi wametumia vitoza machozi kutawanya umati wa watu waliokuwa wamekusanyika nje ya makao makuu ya Idara ya Upelelezi na makosa ya Jinai (DCI) katika Barabara ya Kiambu, Nairobi.

 

Umati unaodaiwa kuwa wafuasi wa aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga, unataka aachiliwe baada ya kujiwasilisha kwa DCI kuhojiwa.

 

Njenga anashikiliwa na polisi baada ya bunduki mbili na zaidi ya misokoto 90 za bangi kupatikana katika nyumba yake moja huko Ngomongo, Kaunti Ndogo ya Bahati.

 

Walioandamana na Njenga ni wakili wake George Wajackoya, kiongozi wa Narc- Kenya Martha Karua, Eugene Wamalwa, na aliyekuwa Gavana wa Murang’a Mwangi wa Iria.

 

Kulingana na Wamalwa, ambaye amezungumza na wanahabari ,Njenga alisafirishwa hadi kusikojulikana huku maswali yakiendelea.

 

Siku ya Jumatano, Njenga alifika katika Mahakama ya Nakuru na baadaye katika afisi za DCI za Kaunti ya Nakuru ambapo alirekodi taarifa.
Aidha alitakiwa kujiwasilisha mbele ya maafisa wa DCI jijini Nairobi leo, kwa uchunguzi zaidi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!