Home » Kenya Yaorodheshwa Kivutio Kikuu Cha Likizo Barani Afrika

Kenya Yaorodheshwa Kivutio Kikuu Cha Likizo Barani Afrika

Kenya ndiyo nchi bora zaidi barani Afrika na ya 10 bora zaidi duniani kutembelea kwa likizo ya kujivinjari, utafiti mpya umefichua.

 

Matokeo ya utafiti yanaweza kuboresha sifa za Kenya kama kivutio cha watalii ambapo utafiti huo uliendeshwa na shirika la Slingo.

 

Maeneo kadhaa ya matukio ya asili kama vile maeneo ya miamba ya matumbawe, kina cha maji na volkano yalizingatiwa kama vigezo vya kupima maeneo ya kuvutia.

 

Kulingana na utafiti huo, Kenya ilitunukiwa pointi 7.26 kati ya 10. Marekani iliorodheshwa kufaa zaidi kwa utalii wa adventure duniani, kwa kupata pointi 9.44 kati ya 10.

 

Ili kuangazia nchi kumi bora zaidi, Kenya inajivunia maeneo mengi kwa vivutio vya asili, ikiwa ni pamoja na volkano 21, 630km2 ya miamba ya matumbawe, sehemu ya juu zaidi ya 5,199m, kina cha maji ambacho kina urefu wa zaidi ya 152m na mbuga 20 za kitaifa.

 

Marekani inayokadiriwa kuwa na volkeno 162, kilomita za mraba 3,770 za eneo la miamba ya matumbawe, sehemu ya juu zaidi ya mita 6,190, kina cha maji 69 ambacho kinazidi urefu wa 152m na mbuga 63 za kitaifa.

 

Mexico inashikilia nafasi ya pili baada ya kupata pointi 8.65 kati ya pointi 10 zinazohitajika huku Japan ikiwa katika nafasi ya tatu kwa pointi 8.39.

 

Katika nafasi ya nne ni Australia yenye pointi 8.25, Ufaransa inashika nafasi ya tano ikiwa na 8.09 huku Ufilipino ikishuka katika nchi ambazo zimefikisha pointi nane kwa pointi 8.06.

 

New Zealand, Costa Rica na Indonesia ziko katika nafasi ya saba, nane na tisa kwa pointi 7.34, 7.30, na 7.29 mtawalia.

 

Australia yenye mbuga 685 za kitaifa inaongoza katika kategoria hii huku Indonesia ikiwa na eneo kubwa zaidi chini ya miamba ya matumbawe yenye kilomita za mraba 51,020.

 

Taifa hilo la Asia pia linaongoza kwa kilele cha mita 4,884 likifuatiwa na Ufaransa iliyo na kilele cha juu zaidi cha mita 4,810.

 

Kenya imedumisha nafasi yake ya juu kama kivutio cha utalii kutokana na kivutio chake cha asili na sekta ya ukarimu iliyochangamka.

 

Wizara ya Utalii inakadiria kuwa mwaka jana kulikuwa na ongezeko la asilimia 83 la mapato yaliyotokana na sekta ya utalii ambayo iliathiriwa zaidi na janga la Covid-19.

 

Nchi ilipata Sh269 bilioni kutokana na utalii mwaka wa 2022 baada ya kupokea watalii milioni 1.5, idadi kubwa zaidi katika kipindi cha baada ya janga hilo na ongezeko la asilimia 70 ikilinganishwa na 2021 waliofika 870,465.

 

Wizara ya utalii ilihusisha ukuaji huo na kuzinduliwa upya kwa huduma za mashirika ya ndege ambapo njia mpya zilianzishwa, kuongezeka kwa masafa ya ndege na kufungua tena misururu ya hoteli za kimataifa.

 

Marekani ilikuwa na watalii wengi zaidi waliopelekwa Kenya ikiwa na asilimia 16 huku majirani zao Uganda wakifuatia kwa asilimia 12.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!