Home » Sifuna: Wakenya Wanapaswa Kupiga Kura Kuhusu Ushuru Wa Nyumba

Sifuna: Wakenya Wanapaswa Kupiga Kura Kuhusu Ushuru Wa Nyumba

Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ametoa maoni kwamba Wakenya wanafaa kuruhusiwa kupigia kura ushuru wa Nyumba uliopendekezwa kwenye Mswada tata wa Fedha wa 2023.

 

Mchango huo uliopendekezwa umekumbwa na mjadala mkali miongoni mwa wakenya na wanachama wa upinzani huku serikali ikijaribu kueleza kwa nini ushuru huo lazima utkelezwe.

 

Akiongea kwenye kipindi cha runinga hii leo Alhamisi, Sifuna amesema kuwa serikali ikiwapotosha wakenya katika kufanya maamuzi yake na imejitahidi kwa urahisi kuwashirikisha wananchi kuhusu jinsi wanavyoweza kupata mapato bila kuzidisha gharama ya maisha.

 

Sifuna ameendelea kudai kuwa nyongeza za ushuru ambazo utawala wa Kenya Kwanza tayari umefanya ni dalili tosha kwamba hawako tayari kushirikisha umma katika mazungumzo yenye kujenga taifa.

 

“Sikiliza mtu, hustler analia anasema naomba usiongeze VAT kwenye mafuta unasema yatapita atake asipende,” alisema.

 

“Hustler anakwambia hawezi kumudu nyongeza ya Ksh.5 kwenye mkate na tayari umepandisha bei ya mkate. Uliwaahidi hawa hustler kuwa unaenda kupunguza bei ya unga, unawadanganya ambapo Unga ni Ksh.150, Ksh.160.”

 

Seneta huyo hata hivyo amewapongeza wananchi ambao wamekuwa wakifanya mikutano kuwasilisha malalamiko yao kuhusu Muswada unaopendekezwa, na kuwataka pia wawe na viongozi kwenye mazungumzo hayo.

 

Akinukuu ibara ya 1 ya katiba ambayo inaeleza uhuru wa wananchi, Sifuna amesema ushuru huo uachwe kwa wananchi kuupigia debe na si wabunge.

 

“Ningetamani hali ambapo Wakenya wenyewe wapewe nafasi ya kupigia kura ushuru huu wa nyumba kwa sababu kama mlivyoona utawala wa sasa ni kiziwi kwetu sote,” alisema.

 

“Badala ya wabunge 290 kupigia kura mswada huu kila eneo bunge linafaa kupigia kura ushuru huu, itapendeza sana.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!