Home » Waziri Kindiki Kusimamia Uchunguzi Wa Miili Ya Shakahola

Waziri Kindiki Kusimamia Uchunguzi Wa Miili Ya Shakahola

Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki leo, Alhamisi, atarejea katika Kaunti ya Kilifi ili kusimamia kuanza kwa shughuli ya uchunguzi wa miili mingine 129 iliyofukuliwa katika msitu wa Shakahola.

 

Miili hiyo ilifukuliwa katika awamu ya pili ya zoezi la ufukuzi wa makaburi ambayo imeshuhudia jumla ya miili 235 ikitolewa msituni hadi sasa.

Shughuli ya uchunguzi wa maiti itafanywa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Malindi.

Miili hiyo inaaminika kuwa ya wahasiriwa wa dhehebu moja linaloongozwa na kasisi Paul Mackenzie Nthenge, mwanzilishi wa Kanisa la Good News International Church, ambaye anadaiwa kuwadanganya waumini wake hadi kufa kwa njaa ‘ili kumpata Mungu’.

Pia sehemu ya ratiba ya Kindiki ni kutembelea Kituo cha Taarifa kwa Umma, Ufuatiliaji na Msaada wa Kijamii kwenye ukingo wa msitu wa Shakahola na Kikosi cha Operesheni ya Utafutaji na Uokoaji ndani ya Msitu huo.

 

Baadaye anatarajiwa kuhutubia taifa kuhusu hali ya mchakato huo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!