Home » Edday Nderitu Awacha Kumfuata Samidoh Instagram

Mkewe Samidoh Muchoki Edday Nderitu amezidisha tetesi za kuachana na matukio yake ya hivi punde.

 

Mama huyo wa watoto watatu amem-unfollow mumewe kwenye Instagram Siku chache baada ya Kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

 

Edday, ambaye alisherehekea siku yake ya kuzaliwa mnamo Jumatatu tarehe 22, hakupokea ujumbe kutoka kwa mumewe.

 

Siku ya akina mama, Samidoh alikuwa miongoni mwa wale waliosusia kabisa kuwaweka kwenye mitandao za kijamii wapenzi wao. Samidoh hakushiriki ujumbe wowote maalum kwa mkewe na mama wa watoto wake watatu Edday Nderitu.

 

Wawili hao wamekuwa wakipitia wakati mgumu kwenye ndoa baada ya Samidoh kuhusika kimapenzi na Seneta Mteule Karen Nyamu.

 

Uamuzi wa Edday wa kuwapeleka watoto wake Marekani ulifuatia kujieleza hadharani kwa uchungu na kufadhaika kuzunguka ndoa yake yenye matatizo na Samidoh.

 

Mnamo Februari 2023, aliingia kwenye mitandao ya kijamii kushiriki hisia zake katika ndoa, akielezea magumu aliyokumbana nayo katika ndoa yake ya miaka 15.

 

Edday alieleza kutokuwa tayari kulea watoto wake katika familia yenye wake wengi, hasa kwa mwanamke ambaye hakuonyesha heshima kwake au kwa familia yake. Aliapa kuendelea kumtanguliza Mungu lakini hangeruhusu watoto wake wavutwe ndani ya bahari ya maumivu.

 

Haijabainika Edday na watoto wake watakuwa Marekani kwa muda gani hata hivyo mashabiki wamekuwa wakimtia moyo kutafuta mapenzi kwingine na kuendelea.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!