Home » Omanga: Azimio Wanavutiwa Na Sava Za IEBC Pekee

Katibu Mkuu wa Utawala katika Wizara ya Masuala ya Ndani Millicent Omanga amedai kuwa chama cha muungano cha Azimio la Umoja-One Kenya kinavutiwa tu na sava za uchaguzi wa 2022 za Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi (IEBC).

 

Katika taarifa yake hii leo Jumatano , Omanga amedai kuwa mazungumzo ya pande mbili kati ya Kenya Kwanza na Azimio yatafeli ikiwa upande wa serikali hautatimiza matakwa ya upinzani.

 

Jana Jumanne, Azimio ilisimamisha mazungumzo ya pande mbili kwa siku saba ikitaja tofauti na ukosefu wa nia njema.

 

Katika taarifa, Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo alisema wawakilishi kutoka upande wa serikali wamekataa kutilia maanani masuala yoyote yaliyopendekezwa na Azimio.

 

Kulingana na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, Kenya Kwanza ilidumisha msimamo mkali kuhusu masuala manne.

 

Muungano wa Azimio unataka mazungumzo yahusu kufungua na kukagua sava za IEBC, kushusha gharama ya maisha na kuwarejesha kazini makamishna wa uchaguzi waliofurushwa baada ya Uchaguzi Mkuu uliopita.

 

Yakijiri hayo, muungano wa azimio hii leo umetishia kuwahimiza wakenya kote nchini kukataa uongozi wa msajili wa vyama Ann Nderitu kwa uongozi mbaya wakidai wakati wa uamuzi kuhusu nani halali wanaongoza chama cha Jubilee alipendelea upande wa Kanini Kega na Sabina Chege ambao wote wako Kenya kwanza

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!