Home » Jackie Matubia Adokeza Kwa Nini Angemwacha Mwanaume Bila Kusita

Jackie Matubia Adokeza Kwa Nini Angemwacha Mwanaume Bila Kusita

Mwigizaji Jackie Matubia amedai kuwa hawezi kuendelea na uhusiano na mwanaume ambaye ameacha kumkimu kimaisha haswaa kifedha.

 

Mwigizaji huyo, kwenye kipande cha picha alichopakia kwenye mtandao wake wa Tiktok akiiga sauti ya mwanamke mwingine, alisema kuwa hawezi hata kufikiria mara mbili juu ya hatima ya uhusiano wake na mwanaume wake, ikiwa mwanaume huyo ataweka kikomo cha kumpa pesa.

 

“Nitamuacha mapema, nitamzuia na kusema kweli siwezi kufanya biashara yoyote na mtu ambaye hataki kunitumia pesa zake. Ni rahisi kama ABC…” Jackie alisema huku akiiga sauti hiyo.

 

Kwa wiki kadhaa sasa, Matubia na mpenzi wake, Blessing Lung’aho wamekuwa wakidaiwa kuwa na msukosuko katika uhusiano wao.

 

Hata hivyo, Matubia katika mahojiano maalum na kituo kimoja cha redio humu nchini alipuuzilia mbali uvumi huo akisema kuwa yeye na Lung’aho walikuwa kwenye ukurasa mmoja lakini pia alionekana kutotaka kueleza kwa kina hali ya uhusiano wao.

 

Mashabiki walianza kukosa raha kuhusiana na uhusiano wao baada ya Matubia kuweka kipande kingine kwenye mtandao wake wa Tiktok akiiga sauti ya mtu ambaye alikuwa ameulizwa uhakika kuhusu uhusiano wao wa kimapenzi na kusema kuwa hana uhakika kabisa na mapenzi.

 

Katika video hiyo, alizungumza kuhusu kosa alilofanya na jinsi ambavyo hangeweza kupona kutokana nalo.

 

“Nilikuwa nikifikiria kuwa mimi ndiye pekee ninayeitwa babyghurl na nilifanya makosa kwa kuchukua simu yake.”

 

Wanandoa hao walianza kuchumbiana mnamo Februari 2021 na hivi karibuni walisherehekea kumbukumbu yao ya ndoa ya pili.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!