Home » Bunge Laonya Kuhusu Mgogoro Unaokuja

Ni lazima nchi itenge fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Mipaka unaotarajiwa mwaka ujao.

 

Haya ni kwa mujibu wa Kamati ya Bunge ya Kitaifa ya Haki na Masuala ya Kisheria ambayo inaonya kuwa huenda nchi ikakumbwa na mzozo iwapo pesa hizo hazitatengwa katika bajeti ya 2023-24 licha ya rasilimali chache.

 

Akizungumza akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya Bajeti, mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Masuala ya Kisheria George Murugara amesema licha ya Tume Huru ya uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutoa ombi la Ksh BILIONI .7.2 ,hakuna pesa zilizotengwa katika bajeti kufikia sasa .

 

Murugara ameonya kuwa kuna hatari ya baadhi ya maeneo bunge kufutiliwa mbali ikiwa zoezi ambalo ni la lazima kwa mujibu wa katiba halitatekelezwa kikamilifu.

 

Murugara pia amedai kuwa IEBC inazama katika deni haswa baada ya kubainika kuwa na ada za kisheria ambazo kwa sasa ni Ksh BILIONI.2.6.

 

Aidha Murugara ametoa changamoto kwa kamati hiyo kuongeza mgao kwa Idara ya Mahakama ili kuendana na ahadi ya Rais William Ruto ya kutoa Ksh BILIONI.3 kwa Idara ya Mahakama kila mwaka wa kifedha.

Awali Rais alikuwa ameahidi kuongeza Ksh BILIONI.3 kwa mgao wa Idara ya Mahakama kila mwaka ambapo kufikia sasa wameongezwa Ksh BILIONI .1 pekee.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!