Home » Rais Ruto: Serikali Kuzindua Vitambulisho Vya Kidijitali

Rais Ruto: Serikali Kuzindua Vitambulisho Vya Kidijitali

Kenya inatarajiwa kuzindua vitambulisho vya kidijitali vyenye data ya kila raia ndio kauli yake Rais William Ruto hii leo Jumatano.

 

Wakati akifungua Mkutano Mkuu wa saba wa (ID-4Africa Augmented General) mjini Nairobi, Ruto aMEsema hii ni sehemu ya mpango wa serikali kuweka mfumo wake wa kidigitali wa usajili wa raia na mfumo muhimu wa takwimu.

 

Kwa mujibu wa rais, serikali pia inataka suluhu la taarifa kamili za abiria wa magari kufuatilia mienendo ya ndani na nje ya nchi.

 

Rais amekaribisha maoni kutoka kwa wataalamu wa usimamizi wa vitambulisho kote nchini unaowezekana ili kufikia ufanisi zaidi katika sekta hiyo.

 

Serikali mwezi Machi ilizindua Kitambulisho cha Kipekee (U.P.I) ili kusajili watoto wote wanaozaliwa wakati wa kuzaliwa na kurekodi visa vya vifo nchini.

 

Katibu Mkuu wa Uhamiaji na Huduma kwa Raia Julius Bittok mnamo Februari alisema U.P.I itawekwa katika tovuti ya e-Citizen na itawapa watoto wote wanaozaliwa nambari ya kipekee ya kutumiwa shuleni na vyuoni.

 

Pia itatumika kama kitambulisho, nambari ya siri, Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya , na Mamlaka ya Mapato ya Kenya, katibu huyo alisema kuwa serikali itaondoa zoezi la sensa kwa kuwa serikali itakuwa na data ya wakati halisi ya idadi ya watu.

 

Kufikia sasa, wanafunzi wa shule za msingi tayari wameanza kupewa U.P.I.s zao katika shule kote nchini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!