Home » KRG Aita Mkutano Na Mama Wa Wanawe Wote

Karuga Kimani maarufu kama KRG the Don alifichuliwa na mwanamke aliyejulikana kama Susan Kinyanjui ambaye alidai kuwa na mtoto wa kike naye kwa jina binti Yvonne mwenye umri wa miaka 19.

 

Akizungumza wakati wa mahojiano na MwanaYouTube Nicholas Kioko, Susan alidai kuwa msanii huyo alimwacha Yvonne naye alipokuwa bado mfanyabiashara katika soko la Gikomba jijini Nairobi.

 

Susan alifichua kwamba alikutana na KRG mwaka wa 2002 alipokuwa na umri mdogo na kudai kuwa mwanamuziki huyo alimpa ujauzito na akajifungua binti yao Yvonne mnamo Agosti 5, 2003.

 

“KRG tulijuana na yeye 2002 akiwa anafanya kazi Gikomba. 2003 August 5 ndo nilipata Yvonne,” “Nilipata mtoi nkiwa under age. Nlikua mdogo sana sikua ata na ID but yeye alikua na ID,” Susan alisema.

 

Susan alidai kwamba KRG alikuwa baba anayewajibika kwa Yvonne alipozaliwa lakini aliacha kumtunza mtoto huyo alipokuwa na umri wa miezi saba baada ya kwenda kuishi na mwanamke mwingine.

 

“Vile nilipata huyu mtoi alikubali mtoto na akaanza kusaidia mtoto ata vitu za hospitali yeye ndo alisimamia kila kitu, manguo za mtoi. Sasa tukakaa after kitu seven months ndo akaanza kuanza kama hataki kulea mtoto after amepata dem mwingine,

 

Mamake Yvonne alisisitiza kuwa KRG ndiye baba mzazi wa binti yake, akiongeza kuwa alikuwa mpenzi wake wa kwanza kabisa.

“KRG ndo baba Yvonne. Nko sure yeye ndo alikua my first boyfriend. Na yeye ndo alisema mtoto aitwe mama yake – Magarette Njoki,”
Susan alidai zaidi kwamba amekuwa akishinikiza KRG kuchukua kipimo cha DNA ili kujua baba wa Yvonne lakini kila mara amekuwa akisusia.

“Bado hatujafanya DNA. Mtoto ni wake yeye ndo alikua my first love. Mtoto ni wake nko sure. Na yeye ndo alikua anafaa akimbie DNA mi ndo namtaka tufanye DNA mbona yeye hatakangi? Nishamwambia tufanye DNA, yeye hatakangi hizo story,”

 

Susan alisema anataka KRG kumlipia karo Yvonne chuoni kwa sababu hana uwezo tena wa kuhudumia elimu yake.

 

Alieleza kuwa alipoteza kazi nchini Sudan na alilazimika kurejea Kenya baada ya vita kuzuka nchini humo.

 

Yvonne alimaliza shule ya upili mwaka jana lakini bado hajajiunga na chuo kikuu kwa sababu mama yake hana uwezo wa kulipia masomo.
Kutokana na video hiyo KRG ameitisha mkutano na wanawake wote wanaodai kuwa na watoto naye baada ya Susan kumfichua kama baba asiyejali watoto wake.

 

“Alooooooh Mambo imechemka Apa 😂😂😂😂 Huyu naona ni Kama ni wa Dufla Kapsa ama Nyinyi Mnaona Kama ni wangu? After God Fear who?

 

“From Next week Kama unadhani Uko na Mtoto wangu we must do a get together ndio tumalize hizi kesi Mara moja Msilete Tena hizi mambo online baadae Tafadhali

 

“But 2002 aaaaiiiiih I was a kid myself bwana!!!! Ama ni post ID kabisa kabisa 😂😂😂😂 #Bughaaa #mamboimechemka,” KRG aliandika.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!