Home » Kakamega:Wanandoa Waliofanya Vasectomy Washangaa Kupata Ujauzito

Kakamega:Wanandoa Waliofanya Vasectomy Washangaa Kupata Ujauzito

Familia moja kutoka kijiji cha Shikoti Kaunti ya Kakamega imepigwa na butwaa baada ya mwanamke mmoja kupata ujauzito licha ya mumewe kufanyiwa upasuaji wa kutolewa mbegu za kiume yaani vasectomy.

 

Medgclay na Beryl, wenye umri wa miaka 36 na 33 mtawalia, walikuwa na watoto watatu walipokubaliana kwamba Medgclay angefanyiwa upasuaji huo katikati ya mwaka jana.

 

Mnamo Julai 12, 2022, alifanyiwa upasuaji huo katika hospitali moja huko Navakholo, zoezi lililofanywa na madaktari wa eneo hilo kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali.

 

Miezi 12 baadaye, wawili hao sasa wanatarajia kupata mtoto wa nne Juni mwaka huu bila kujua nini kilifanyika kwa zoezi hilo ambalo waliamini lingewasaidia kupanga familia zao, hasa katika wakati mgumu wa kiuchumi.

 

Mnamo Novemba, Beryl alikosa hedhi, jambo ambalo wenzi hao walisema walilipuuza kuwa ni tukio la hedhi isiyo ya kawaida.
Mnamo Desemba, waliarifiwa kwamba walikuwa wanatarajia mtoto wao wa nne.

 

Kwa mujibu wa Dora Amakobe, daktari aliyefanikisha taratibu za kufunga uzazi kwa wanaume, kuna uwezekano wa njia hiyo kushindwa iwapo mgonjwa hatafuata maelekezo kamili ya daktari, ikiwamo kutofanya mapenzi bila kinga kwa zaidi ya miezi mitatu.

 

Beryl anasema katika yote haya, hakujawa na masuala ya usaliti kati yake na mumewe.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!