Home » Yanga yatinga Fainali CAFCC

 

Hayawi hayawi sasa yamekua. Hili limejiri baada ya mabingwa wa ligi kuu nchini Tanzania Yanga kutinga Fainali CAFCC baada ya kumtoa Marumo Gallants kwa ujumla wa mabao 4-1.

 

SOMA PIA:Yanga Mabingwa Ligi Kuu NBC

 

Hatua hiyo ya fainali imejiri ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu kutokea Tanzania kufika katika fainali za kombe la shirikisho (CAFCC) tangu kuanzishwa kwake.

 

 

Katika kuisaka hatua ya fainali za kombe la shirikisho Yanga pamoja na Marumo Gallants walipita katika mizunguko miwili, ikiwemo mechi ya nyumbani pamoja na ugenini.

 

Mchezo wa kwanza ni ule uliofanyika katika uwanja wa Mkapa na Yanga kushinda mabao 2-0 na mechi ya pili ni baada ya Marumo kukubali kichapo cha bao 2-1 walipokuwa katika uwanja wa nyumbani wa Royal Bafokeng.

 

Katika hatua ya Fainali, Yanga watavaana na USM Alger ambao  walimuondoa ASEC Mimosas katika hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa bao 2-0

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!