Home » Mamake Gavana Wa Benki Kuu Ya Kenya Afariki Dunia

Mary Agnes Njambi, mamake Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Dkt Patrick Njoroge na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Anthony Muheria amefariki dunia.

 

Familia ya Bi Njambi imeambia wanahabari leo Jumatatu jioni kwamba mama huyo amefariki alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kwa muda mrefu.

 

Aidha kabla ya kifo chake Mama Njambi amekuwa na kazi nyingi kama mwalimu na vile vile mtaalum.

 

Mary aliolewa na Thomas Ngugi na walikuwa na watoto wanane.

 

Familia yake imemtaja kama kiongozi bora na mlezi wa Kikatoliki na mhamasishaji wa jamii ambaye alivumilia ugonjwa wake kwa ushujaa mkubwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!