Gachagua Atetea Uteuzi Wa Serikali Akimshambulia Raila

Naibu Rais Rigathi Gachagua ametetea uteuzi uliokumbwa na utata katika utawala wa Rais William Ruto wakati ya mazishi ya mkewe Dedan Kimathi, Mukami Kimathi ambaye amezikwa kaunti ya Nyandarua.kutambuliwa kwani walimpigia kura nyingi rais Ruto.
Naibu rais amedai kuwa wakazi wengi kutoka eneo la Mlima Kenya walikuwa wakitumikia vifungo katika Gereza la Kamiti Maximum, lakini wakosoaji walilenga walioteuliwa na serikali badala ya kuwatetea wafungwa.
Wakati huo huo, ameendeleza mashambulizi yake dhidi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga akiwahutubia wahutubia waombolezaji, Gachagua amemsuta Raila, akimtaja kwa kuongoza maandamano dhidi ya serikali kuhusu gharama ya maisha.
Awali Raila alikuwa amemkashifu Gachagua kwa kutoa maagizo kuhusu mazishi ya Mukami kuwa ya kitaifa licha ya kutoshuhudia bendera kukupeperushwa nusu mlingoti.
Raila amekashifu zaidi utawala wa Ruto kwa kukosa kuheshimu matakwa ya mwisho ya Mukami ya kuzikwa pamoja na marehemu mumewe, Dedan Kimathi.
Ruto, akijibu, ameahidi kushughulikia maswala ya ardhi yaliyoibuliwa na Raila na Gachagua na kuanzisha jumba la makumbusho la kumuenzi Mukami na watetezi wengine wa uhuru na kufuatilia mabaki ya Dedan Kimathi kwa uwasilishaji bora.