Home » Mwili Wa Mwanaume Wapatikana Umetupwa Kando Ya Barabara Nakuru

Mwili Wa Mwanaume Wapatikana Umetupwa Kando Ya Barabara Nakuru

Mwanaume wa miaka 48 ambaye alitoweka siku nne zilizopita amepatikana leo hii Jumamosi akiwa amefariki na mwili wake kutupwa kando ya barabara Kaunti ya Nakuru.

 

Aidha ni Watoto wa shule waliopata mwili huo ukiwa umetupwa kando ya barabara.

 

Marehemu ametambuliwa kama Geoffrey Bett, 48 ambaye alitoweka siku ya Jumanne.

 

Aidha maafisa wa Polisi wamesema mwili huo ulikuwa na majeraha kadhaa yanayoshukiwa kuwa ya kisu.

 

Familia ilitilia shaka waliposhindwa kumuona Bet kwa siku mbili na kuamua kuthibitisha ugunduzi huo, na kukuta mwili huo ukiwa barabarani ukiwa na kamba shingoni.

 

Mwili huo uligunduliwa mita chache kutoka mahali ambapo mwili wa mwanamke ulipatikana umetupwa wiki iliyopita

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!