Home » Gavana Badilisha Apendekeza Historia Ya Mau Mau Kuhifadhiwa

Gavana wa Nyandarua Kiarie Badilisha amependekeza kujengwa jumba la makumbusho la Mau Mau ili kuweka kumbukumbu za mapambano ya kupigania uhuru.

 

Akizungumza Badilisha amebainisha kuwa kaunti hiyo ina historia tele ya vuguvugu hilo ambalo lilikuwa na jukumu muhimu katika uhuru wa Kenya.

 

Gavana amesema tayari serikali ya kaunti imeanza kuweka kumbukumbu za matukio ya Mau Mau.

 

Mau mau ni vuguvugu la wenyeji lililokuwa limeanza kuasi utawala wa kikoloni wa Uingereza, ambao ulikuwa umetawala eneo hilo tangu 1895.

 

Harakati hizo zilijumuisha Wakikuyu, kabila kubwa zaidi la asili la Kenya, ambao wengi wao walikuwa wameondolewa kwenye ardhi yao yenye rutuba katika eneo la mlima Kenya na wakoloni.

 

Uasi wa Mau Mau ulianza mwaka wa 1952 kama majibu ya ukosefu wa usawa wa haki katika Kenya inayotawaliwa na Waingereza.

 

Mbali na hayo rais William ruto amewapongeza viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo vile vile waliochangia serikali ya majimbo kubuniwa na kufanya taifa hili kusonga mbele kidemokrasia huku akimkumbuka Mama Kimathi kama aliyetoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru wa taifa la kenya.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!