Home » DCI Waanzisha Uchunguzi Kuhusu Kuibiwa Kwa Mwinjoyo FM Nakuru

DCI Waanzisha Uchunguzi Kuhusu Kuibiwa Kwa Mwinjoyo FM Nakuru

Idara ya Upelelezi na makosa ya Jinai (DCI) leo hii Jumamosi, imeanzisha msako wa kuwasaka washukiwa waliovamia kituo cha redio cha Injili chenye makao yake mjini Nakuru cha Mwinjoyo FM.

 

Kulingana na DCI, kundi hilo la watu wanne lilichukua simu nane, pesa taslimu zaidi ya Ksh elfu 35,000 na aina nane za viatu.

 

Maafisa wa upelelezi katika Kaunti ya Nakuru wameomba taarifa kutoka kwa umma kusaidia kuwakamata washukiwa hao.

 

Katika video hiyo ya dakika tatu, mmoja wa wahalifu hao alikuwa na bunduki na panga, huku mwingine akiwa na bunduki pekee.

 

Wawili hao waliendelea kukagua lango la kuingilia iwapo wangevamiwa wakati wa uvamizi huo na kutoweka na vifaa kadha vya kituo hicho cha redio.

 

Kwa sasa maswali yameibuliwa na wakazi wa maeneo hayo wakishangaa jinsi kituo kama hicho kinaweza kuvamiwa kwa takriban dakika kumi na tano bila maafisa wa polisi kufika eneo la tukio na kuwakibili.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!