Home » Sylvanus Osoro: Tutapitisha Mswada wa Fedha, Serikali Haipotezi

Sylvanus Osoro: Tutapitisha Mswada wa Fedha, Serikali Haipotezi

Mbunge wa Mugirango Kusini na kinara wa walio wengi katika Bunge la Kitaifa Sylvanus Osoro amesema Bunge litapitisha Mswada wa Sheria ya Fedha wa 2023 bila kubadilisha chochote ndani yake.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha waziri wa Ulinzi Aden Duale, Osoro alisema kwamba mipango ya serikali ya siku hiyo lazima ipite kila wakati, na hivyo kuongeza kuwa hata Mswada wa Fedha utapitishwa kwa urahisi.

 

Matamshi ya mbunge huyo yanajiri siku chache baada ya Seneta wa Nandi Samson Cherargei kutupilia mbali malalamiko ya umma na kusema Bunge litapitisha Mswada wa Fedha uliopendekezwa kwa ukamilifu.

 

Seneta huyo alipuuzilia mbali Wakenya wanaolalamikia kuchunguzwa kwa Mswada huo, akisema kuwa ushuru umeongezwa tu kwa bidhaa za kifahari.

 

Mswada huo unaolenga kuongeza ushuru kwa bidhaa mbalimbali ambazo ni pamoja na vipodozi vya wanawake, kucha bandia na bidhaa nyingine za urembo umezua taharuki miongoni mwa viongozi wa upinzani pamoja na vyama vya wafanyakazi na waajiri wao.

 

Katibu Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu vya Kenya (KUSU) Charles Mukhwaya alisema Mswada huo utaongeza makato ya kisheria ya wafanyikazi ikiwa utapitishwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!