Home » Kajala, Paula Waja Na Behind The Gram

 

Mwigizaji Kajala pamoja na mtoto wake Paula waja na reality Show Yao waliyoipa jina la Behind The Gram iliyozinduliwa siku za hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency iliyopo katika viunga vya jiji la Dar es salaam.

 

SOMA PIA:Marioo, Paula Wazama Penzini

 

Katika ujio wa Behind the Gram mashabiki wa Paula pamoja na Kajala watapata nafasi ya kuona maisha yao kwa undani zaidi, visa, kazi pamoja na harakati zingine za kimaisha kuwahusu wao.

 

Uzinduzi wa Behind the Gram ulihudhuriwa na watu maarufu waliofika katika kuwafunga mkono. Baadhi ya watu walihudhuria katika uzinduzi huo ni pamoja na nyota wa muziki Marioo, Mc Garab, Phina, Aunt Ezakiel, Zamaradi Mketema pamoja na wengine wengi.

 

Reality show hiyo itakuwa ikirushwa hewani siku za Jumatano kupitia chaneli ya Zamaradi TV iliyopo katika king’amuzi cha Azam chaneli 413 na kurudiwa siku ya Alhamis.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!