Home » TANZIA : Bernard Membe Afariki Dunia

Bernard Membe Afariki DUNIA

 

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa nchini Tanzania Bernard Membe afariki dunia siku ya Ijumaa asubuhi katika hospitali ya Kairuki iliyopo  jijini Dar es Salaam.

 

SOMA PIA:Mwanamuziki Maarufu Gloria Bossman Afariki Dunia

 

Chanzo cha kifo Cha Membe ambaye alikuwa pia mbunge wa jimbo la Mtama kimetajwa kuwa ni kifua kilichombana majira ya usiku na kupelekea hospitalini licha ya jitihada zote lakini mauti yalimkuta.

 

Baada ya taarifa za kifo kusambaa, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dtk. Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole na kumsifu Membe kama moja ya viongozi walipokuwa mahiri.

 

 

Licha ya kuwa Waziri wa Mambo ya nje lakini pia Bernard Membe alikuwa Moja ya viongozi waliokuwa wakiwania nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka 2020 kupitia Chama Cha ACT – Wazalendo.

 

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe……..

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!