Home » Vileo Ghushi Vyanaswa Nakuru.

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Leo hii Alhamisi imeripoti kunasa kwa vileo visivyolipiwa ushuru vinavyokadiriwa kugharimu Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA) KShilingi elfu mia 342,482.

 

Kulingana na DCI Vinywaji vileo vilivyokamatwa katika kaunti ya Nakuru viliripotiwa kuwa vimefungwa kwenye katoni zaidi ya mia 120.
Hatua hiyo inajiri wakati Naibu Rais Rigathi Gachagua akiongoza juhudi za kukabiliana na utumizi wa dawa za kulevya na ulevi ambao umekithiri katika eneo la mlima kenya.

 

Aidha naibu rais Gachagua amewaagiza wasimamizi wa serikali ya kitaifa katika ngazi ya mikoa na kaunti kukabiliana na pombe haramu kila sehemu.

 

Naibu rais pia ametoa wito kwa serikali za kaunti kudhibiti utoaji wa leseni za baa, akisema unywaji wa pombe haramu umefikia viwango vya kutia wasiwasi na unatishia kuondoa kizazi kijacho haswa katika eneo la Kati mwa Kenya.

 

Gachagua kufikia sasa amefanya mikutano kadhaa ya mashauriano kuhusu Kukabiliana na Ulevi akionyesha zaidi hatua ya serikali ya kujenga vituo vya kurekebisha tabia katika kaunti zote ili kukabiliana na matumizi mabaya ya dawa za kulevya na pombe.

 

Gachagua anatarajiwa kuandaa kongamano la kudhibiti pombe haramu na dawa za kulevya huko Nakuru, Mombasa, Kakamega na Embu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!