Home » KeNHA Yaonya Umma Kuhusu Nyufa Kwenye Barabara Ya Mai Mahiu-Rironi

KeNHA Yaonya Umma Kuhusu Nyufa Kwenye Barabara Ya Mai Mahiu-Rironi

Mamlaka ya Kitaifa ya usalama Barabarani (KeNHA) imetahadharisha umma kuhusu nyufa kwenye Barabara ya Mai Mahiu-Rironi yenye shughuli nyingi.

 

Katika taarifa yake, mamlaka hiyo imebainisha kuwa msukosuko huo uliokuwa ukiendelea kutoka mchana ulitokana na lori kubingiria mara kadhaa katika barabara hiyo.

 

Barabara hiyo inaunganisha Naivasha, Mai Mahiu na Nakuru, hadi Bohari ya Kontena ya Ndani (ICD) na Hifadhi ya Viwanda huko Naivasha.
Aidha barabara hiyo vile vile ina idadi kubwa ya watu wengi zaidi na malori ya kupita, pia ina jukumu kubwa la kiunganishi kwa trafiki inayoenda maeneo ya mbali kama vile Narok, Kusini Magharibi mwa Kenya na Kaskazini mwa Tanzania.

 

Eneo la Mai Mahiu limekumbwa na majanga ya kimazingira, ikiwa ni pamoja na nyufa kali zilizotokea kwenye njia ya Mai-Mahiu – Narok na kulazimisha KeNHA kufunga barabara hiyo kwa siku nne tangu Jumapili, Aprili 30.

 

Wakati wa kufungwa, waendeshaji magari walielekezwa kwenye njia ndefu zaidi ili kupisha njia za ukarabati wa wahandisi kutoka mamlaka hiyo.

 

Nyufa hizo zilisababishwa na mvua kubwa iliyonyesha eneo hilo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!