Home » Yesu Wa Tongaren Akamatwa

Maafisa wa Polisi kwa sasa wamemzuilia Eliud Wekesa, maarufu kama Yesu wa Tongaren, saa chache baada ya kumhoji katika Makao Makuu ya Idara ya upelelezi na makosa ya jinai DCI tawi la Bungoma.

 

Yesu wa Tongaren anatarajiwa kufikishwa mahakamani huku maafisa wa DCI wakiomba maagizo ya mahakama ya kumzuilia kwa siku zaidi.

 

Maafisa wa Polisi wameongeza kuwa walikuwa wamepanga kupeleka faili yake kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) ili kushauriwa kuhusu jinsi ya kuendelea na shughuli hiyo.

 

Kulingana na Wekesa, aliwashawishi polisi kwamba watoto walio chini ya uongozi wake wanahudhuria shule na kutibiwa hospitalini inavyotakiwa kisheria.

 

Kuhusu iwapo kanisa lake liliandikishwa, anavyojiita, Yesu alieleza kwamba mchakato huo ulikuwa ukiendelea.

 

Awali Kiongozi huyo wa Kanisa la New Jerusalem alikariri kwamba hakuwa na hatia na alikuwa mtu wa Mungu ambaye hajihusishi na uhalifu.

 

Mnamo Alhamisi, Mei 4, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale aliwataka polisi mjini Bungoma kuwachunguza wachungaji wanaodaiwa kuwapotosha waumini Magharibi mwa Kenya.

 

Yakijiri hayo…Viongozi wa kidini kutoka kilifi wameitaka Wizara ya Usalama kuweka juhudi zaidi ili kuwaokoa walioko katika msitu wa shakahola.

 

Hii ni baada ya waziri Kithure Kindiki kukiri kuwa baadhi ya wafuasi wa Paul Mackenzie wamebadilisha mbinu ya kujificha msituni.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!