Home » Justina Syokau Afichua Sababu Ya Kuwa Single

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Justina Syokau hatimaye amefichua sababu ya kuwa single kwa takriban muongo mmoja.

 

Katika mahojiano na Mungai Eve siku ya Jumatatu, mama huyo wa mtoto mmoja alisema kuwa wanaume wengi wamekuwa wakimuacha baada ya kuwaambia kuwa ana mtoto.

 

“Mi nina mtoto mmoja na nina miaka kumi hapa nje pekee yangu. Unakuta tukipatana na watu pale nje watu wanakataa mtoto tu mmoja.”
Kulingana na Syokau, amekataliwa mara nyingi kwa sababu ana mtoto.

 

“Nimekaliwa mara mingi. Wakati unaambia mwanaume uko na mtoto anaona ni burden. Unakuta alikuwa na appetite ya kuwa na wewe, alikua na mpango anataka kukuoa. The moment unamwambia ni single mother uko na unaona ameboeka.”

 

Msanii huyo alisema kuwa baadhi ya wanawake wanaolea watoto peke yao hawakuchagua hivyo bali walijikuta tu.

 

“So kuwa na mtoto si kuwa na maisha mabaya. At least mimi nilikuwa nimeolewa. Kuna mtu alipata mimba class eight na amesoma hadi university, huwezi kataa msichana yule juu hajaolewa.”

 

Justina alifichua kuwa anampenda Akothee kwa sababu ni mchapakazi, licha ya kuwa ‘mama mmoja’.

 

“Amekuwa rais wa single mothers na mimi ni single mother. Anaeza kuwa hajaokoka lakini Akothee nampenda juu ako na bidii,” alisema.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!