Nyokabi: Uhuru Hawezi Staafu
Aliyekuwa mwakilishi wa Wanawake wa Nyeri, Priscilla Nyokabi amesema kuwa aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta hawezi kustaafu kisiasa wakati chama chake kiko kwenye mtafaruku.
Nyokabi amesema japo itakuwa vyema iwapo rais huyo mstaafu atastaafu kutoka kwa siasa kali, anahitaji kuwa na chama cha Jubilee kwa utaratibu na kudai kuwa jinsi mambo yalivyo, ni Uhuru pekee ndiye anayeweza kutatua tatizo linalokisumbua chama tawala cha zamani.
Nyokabi ambaye ni mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi pia amesema anatumai Uhuru atasuluhisha vita vya ndani ambavyo chama kimekumbana nacho hivi majuzi na kuacha mifumo inayoweza kutatua masuala yoyote kama hayo ambayo yanaweza kutokea siku zijazo.
Kulingana na Nyokabi ingawa sheria inasema mkuu wa nchi aliyestaafu hafai kushikilia wadhifa wa kisiasa miezi sita baada ya kuondoka madarakani, baadhi ya vipengee vya Katiba vinamruhusu.
Kumekuwa na wito kutoka Kenya Kwanza kumtaka Uhuru astaafu kutoka kwa siasa kali.