Home » Felix Koskei:Hakuna Mali Itaharibiwa Wakati Wa Maandamano

Felix Koskei:Hakuna Mali Itaharibiwa Wakati Wa Maandamano

Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei amesema kuwa mashirika ya usalama yameagizwa kulinda maisha na mali ya Wakenya huku maandamano ya Azimio yakitarajiwa kuanza tena.

 

Akizungumza katika Chuo cha Kapsabet wakati wa hafla ya kustaafu ya askofu msaidizi wa A.IC. Benjamin Samoei, Koskei amesema kuwa vyombo vya usalama vitahakikisha kuwa hakuna mali inayoharibiwa wakati wa maandamano dhidi ya serikali.

 

Koskei amewahakikishia Wakenya kwamba serikali haitavumilia uvunjaji sheria wowote, akishikilia kuwa maisha ya watu pia yatalindwa.

 

Koskei ameongeza kuwa katiba inaruhusu kila mtu kufanya maandamano, akibainisha kuwa yeyote anayevuruga amani atakabiliwa na sheria.

 

Mkuu huyo ametoa wito kwa viongozi wote kuhamasisha Wakenya kufanya masuala ya maendeleo badala ya kushiriki maandamano kila mara jambo ambalo linaaminika kuathiri uchumi.

 

Azimio imetangaza kuwa watafanya maandamano kesho Jumanne licha ya polisi kukataa kuwaruhusu.

 

Kupitia taarifa ya Jumapili, kiongozi wa Azimio Raila Odinga alitangaza kwamba watawasilisha maombi katika afisi nne za serikali katika juhudi za kushinikiza utawala wa Rais William Ruto kutii matakwa yao.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!