Home » Kindiki Kwa Maseneta: Majambazi Hawana Nafasi Nchini Kenya

Kindiki Kwa Maseneta: Majambazi Hawana Nafasi Nchini Kenya

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki ametaja operesheni ya usalama iliyoanzishwa miezi miwili iliyopita ili kuwaondoa majambazi katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya kukumbwa na changamoto mbalimbali.

 

Kindiki ambaye ni Waziri wa kwanza kujitokeza rasmi leo hii Jumatano mbele ya Seneti kufuatia marekebisho ya Kanuni za Kudumu hata hivyo anasikitika kwamba bado kuna mapungufu ambayo yatachukua muda kuyarekebisha.

 

Akijibu maswali ya Maseneta kuhusiana na hali ya usalama nchini, Kindiki amedai kwamba wanajeshi na maafisa wa polisi watasalia katika maeneo yanayolengwa hadi tishio hilo litakapotokomezwa.

 

Aidha, Waziri Kindiki amewahakikishia maseneta kwamba operesheni hiyo ya pamoja itafanikishwa hivi karibuni .

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!