Home » Zuchu Awafunika Tiwa Savage Na Ayra Starr
Zuchu Boomplay

Kutoka nchini Tanzania, msanii kutokea lebo ya WCB Wasafi, Zuchu ameweka rekodi mpya kwenye muziki wake baada ya kwa mara nyingine kuwafunika wasanii wakubwa kutoka Nigeria, Tiwa Savage na Ayra Starr. 

 

 

Soma Pia: Zuchu Avunja Rekodi Golden Club Boomplay

Zuchu ambaye hivi karibuni amekuwa ni msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki kufikisha streams Milioni 200 Boomplay ameweka rekodi mpya kwenye mtandao huo wa kusikiliza na kupakua muziki. 

Zuchu - YouTube

Kwenye app ya Boomplay, Zuchu ndiye msanii wa kike anayeongoza kwa kuwa na nyimbo nyingi zaidi zilizofikisha streams Milioni 10 akiwa na nyimbo 6 zilizofikisha idadi hiyo ya streams huku Tiwa Savage na Ayra Starr wakiwa na nyimbo mbili tu zilizofikisha streams Milioni 10. 

 

Nyimbo za Zuchu zilizofikisha streams Milioni 10 Boomplay ni pamoja na Fire, Kwikwi, Sukari, Utaniua, Mwambieni na Love.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!