Home » Makala: Mambo 5 Usiyoyajua Kuhusu Msanii Cherry

Makala: Mambo 5 Usiyoyajua Kuhusu Msanii Cherry

Cherry Singer Biography

Kama unafuatilia muziki kutoka Tanzania basi bila shaka utakuwa unamfahamu Cherry, msanii mpya kabisa katika kiwanda cha Bongo Fleva ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa kuitwa “Closer”. 

 

Kwenye kiwanda ambacho kwa sasa kina ushindani mkubwa wa kimuziki, bila shaka Cherry amejitengenezea nafasi yake kwenye soko la Bongo Fleva huku akitesa na mtindo wake kuchanganya RnB na Afrobeats. 

Cherry Biography

Haya hapa ni mambo matano usiyoyajua kuhusu wasifu (biography) ya msanii Cherry: 

Ameshashiriki Mashindano Ya Bongo Star Search 

Bongo Star Search ni moja kati ya mashindano makubwa ya kusaka vipaji vya muziki nchini Tanzania na kwenye msimu wa 11 wa shindano hilo, Cherry alifanikiwa kushiriki mpaka kuingia kwenye kumi bora yaani Top 10. 

Soma Pia: Zuchu Avunja Rekodi Golden Club Boomplay

Kwa mujibu wa Cherry alidokeza kuwa, rafiki jirani yake ndiye aliyemshawishi kushiriki mashindano hayo baada ya kumsikia akiimba wakati anafanya kazi zake za ndani. 

 

Maisha Ya Mapema 

Cherry amezaliwa huko mkoani Kilimanjaro na alianza kuimba kanisani pindi akiwa mdogo sana. Ukiweka kando kipaji chake, Cherry pia ni msomi ambapo alisoma kwenye chuo cha Kairuki Dar Es Salaam ambapo alikuwa anasomea uuguzi na ukunga kwa ngazi ya Diploma. 

Cherry Msanii Wa Tanzania

 

Ametengeneza Historia 

Kama moja ya kazi zake za kwanza kabisa kwenye muziki, Cherry alichaguliwa kushiriki kutengeneza EP maalum kwa ajili ya filamu ya “Love Transfusion” kitu ambacho ni nadra sana kutokea hasa kwa msanii ambaye ndio kwanza anaingia kwenye “game”

 

Love Transfusion ni EP yenye ngoma nne ambazo ni “Closer”, “Kiapo Cha Damu”, “Nikikupata” pamoja na “Nimekubali” 

 

Amesainiwa B Extra Records

Ili kuweza kujipeleka mbele zaidi, Cherry alijiunga na B Xtra lebo ambayo inamilikiwa na producer wa muziki, Hermy B ambaye amehusika  kutengeneza hits tofauti tofauti kwenye uwanja wa Bongo Fleva ikiwemo wimbo wa kwanza kabisa wa Vanessa Mdee wa kuitwa “Closer” 

Cherry Singer Biography

 

Wasanii Waliomshawishi

Kitu kingine usichokijua kwenye Biography ya msanii huyu ni kwamba, Cherry amewataja wasanii kama Beyonce kutoka Marekani, Tems kutoka nchini Nigeria na Lady Jaydee kutoka nchini Tanzania kama wasanii anaowaangalia zaidi na ambao wamefinyanga aina ya muziki anaofanya. 

 

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!