Home » Diamond Platnumz Na Shilole Wateuliwa Na Rais Samia
Diamond Platnumz Shilole

Wasanii kutoka nchini Tanzania, Diamond Platnumz na Shilole maarufu kama Shishi Baby wameingia kwenye vichwa vya habari Tanzania baada ya kuteuliwa na Rais Samia. 

 

Platnumz na Shilole ni kati ya wasanii wenye wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram ambapo Diamond Platnumz anaongoza akiwa na Milioni 15 huku Shilole akiongoza kwa upande wa wanawake akiwa na Milioni 9.8 

 

Hivi karibuni, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu  katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani Kitaifa Ametangaza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan Amewateua Wasanii na Wafanyabiashara Diamond na Shishi kuwa Wajumbe na Mabalozi wa Kupambana na Ugonjwa wa Malaria.

 

Soma  Zaidi: Diamond Amzawidi Mfanyakazi Wake Gari Na Kipande Cha Ardhi

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shilole ameshukuru kwa kupata nafasi ya kuwa balozi na kuongeza kuwa ataifanya kazi hiyo kwa ukamilifu mkubwa. 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!