Home » Wanaume Wawili Wafariki Nyeri Katika Vita Vya Deni La Shilingi Ishirini

Wanaume Wawili Wafariki Nyeri Katika Vita Vya Deni La Shilingi Ishirini

Wanaume wawili wametangazwa kufariki katika mji wa Nyeri baada ya mzozo kuhusu kile kinachosemekana kuwa deni la shilingi 20.

 

Kulingana na ripoti ya polisi, Kelvin Wachira alidungwa kisu shingoni na mwanamume aliyejulikana kwa jina la Githinji pekee katika vita hivyo vilivyozuka baada ya wawili hao kudaiwa kutofautiana kuhusu jinsi deni hilo lingetatuliwa.

 

Githinji alijaribu kutoweka kutoka eneo la tukio muda mfupi baadaye lakini alinaswa na umati uliomvamia, kulingana na walioshuhudia.

 

Wawili hao baadaye walitangazwa kufariki kando-kando katika Hospitali Kuu ya Nyeri ambapo walikuwa wamekimbizwa kwa matibabu.

Miili yao imepelekwa katika Hifadhi ya Maiti ya Hospitali ya Rufaa ya Nyeri.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!