Home » NCCK Yataka Kurejeshwa Kwa Uhakiki Wa Mashirika Ya Kidini

NCCK Yataka Kurejeshwa Kwa Uhakiki Wa Mashirika Ya Kidini

Makasisi wa kanisa katoliki wametaka uchunguzi wa kina ufanywe kuhusu vifo vya zaidi ya watu 90 katika kaunti ya Kilifi.

 

Askofu Mkuu Martin Kivuva amesema kuwa inasikitisha kwamba taifa linashuhudia hali inayotia wasiwasi ambapo wale wanaojiita manabii na viongozi wa kidini wamebobea katika kuwanyonya Wakenya wanyonge kwa jina la dini.

 

Aidha amebainisha kuwa baadhi ya wafuasi wasio na hatia wamepoteza pesa, mali na kuwataka Wakenya kuwa macho kila wakati.

 

Maaskofu hao wamekubali changamoto ya kujitawala katika mazingira ambapo madhehebu mengi yanapinga miundo na mifumo ya uongozi.
Kulingana nao kama nchi ingekuwa na utaratibu wa kudhibiti dini.

 

Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Makanisa ya Kenya (NCCK) Chris Kinyanjui amesema makasis tapeli wako tayari kupotosha umati kwa kuwapa mafunzo potovu.

 

Kinyanjui amesema Msajili wa Vyama ameacha kushauriana na NCCK na kusababisha kuongezeka kwa makanisa ambayo ukweli na uaminifu wake unatiliwa shaka.

 

Siku ya Jumatatu, Kanisa la Christ Is The Answer Ministries (Citam) lilitoa changamoto kwa serikali kufanya uchunguzi ufaao kuhusiana na suala tata la shakahola kaunti ya kilifi linamhusu Kasis Paul Mackenzie.

 

Kwa upande mwingine Wanasiasa wamekosoa mafundisho ya kitamaduni ambayo yanaonekana kupotosha waumi na viongozi mbalimbalu huko Shakahola.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!