Home » Majizzo Na Utambulisho Mpya Wa Kibunifu

 

Ukurasa mpya wa vyombo vya habari Tanzania umechukua nafasi baada ya wamiliki wa radio kubwa nchini kufanya mageuzi ya kushtukiza. Mageuzi hayo yamefanyika katika vyombo vya habari haswa katika redio. Kwa upande wa ubunifu mmiliki wa E Media, Majizzo ameanza kivingine baada ya kumtambulisha Masanja Mkandamizaji  EFM kwa staili ya utofauti ambayo haikutarajiwa .

 

SOMA PIA:Saida Mouh Akana kufahamu Umiliki Wa Mali Za Achraf Hakimi

 

Ubunifu huo ulionekana mara baada ya Majizzo kuchapisha video katika ukurasa wake wa Instagram. Video hiyo iliyobeba ujumbe mzito ambayo ilionesha matendo na harakati mbalimbali za maisha ya kila siku. Mtendo hayo yenye mitikasi ya hapa na pale yanamuonesha Majizzo akiwa mhusika mkuu.

 

Kwanza video ilianza kumuonesha Majizzo akibeba uhusika wa muendesha bodaboda akiwa kijiweni. Simu ikaita na baada ya kuipokea ikamlazimu kuondoka eneo lile kwa haraka zaidi. Safari yake hiyo aliyoianza ilikuwa na mikasa mingi ambayo yote alitakiwa kuikamilisha kabla ya kufikia lengo husika la simu iliyoita

 

Mkasa wa kwanza ni pamoja na maji yaliyotwama ambayo hayakumzuia Majizo kufika mahali alipohitaji, baada ya hapo kuna mama mjamzito ambaye alitakiwa kumfikisha zahanati kwa ajili ya hudumu baada ya usafiri wake kupata hitilafu. Barabara iliyozibwa nayo pia ni moja ya kikwazo alichokumbana nacho Majizzo kabla ya kumfikia abiria wake. Abiria huyo si mwingine bali ni Masanja mkandamiza na kumfikisha makao makuu ya E Media. Hili ndilo lengo la safari hiyo na hatimaye wanakutana na mwenyeji wao akionekana na mzee mwenye wadhifa. Mzee huyo anaonekana akimkabidhi Masanja Magazeti kwa ajili ya kuanza kazi.

 

Hii ni ni stori ambayo imebeba taswira kwa Majizzo ikimaanisha ya kuwa katika safari yake ya kuwa mmiliki wa chombo kikubwa cha habari kama E Media. Matukio mengi pamoja na mikasa ambayo alipitia na hatimaye kifikia lengo lake ikiwemo kuweka ubunifu na kusaka vipaji vipya katika tasnia ya vyombo ya habari Tanzania.

 

Tukio la utambulisho wa Masanja katika viunga vya E Media limezua taharuki kubwa katika vyombo vya habari. Hili limejiri haswa baada ya mtangazaji huyo kutoka katika kituo cha habari cha Wasafi FM na kuhamia E FM.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!