Home » Mwambie Afungue Server! Mchungaji Ng’ang’a Awaambia Wanaume

Mwambie Afungue Server! Mchungaji Ng’ang’a Awaambia Wanaume

Mchungaji wa Neno Evangelist James Ng’ang’a amewataka wakenya kukesha.

 

Kwa mujibu wa Ng’ang’a, wanawake wamekuwa wakivaa viboreshaji ili kuifanya miili yao haswa ionekane kubwa na ya mviringo.

 

Ng’ang’a aliwashauri wanaume kuomba ‘server’ hiyo ifunguliwe ili kuthibitisha ikiwa nyash ni halali au la.

 

“Wanaume wacha niwasaidie,hizi manyuma nyuma unaona wako nazo si nyuma mwambie fungua nione. Kuna nguo zinashonwa zakumeesha manyuma nyuma,mgu ni ndogo huku juu ni ndogo mwambie fungua nione.”

 

Hivi majuzi video ya Mchungaji Ng’ang’a akiwalipua wake wa kwanza kwenye ugomvi na vifaranga wa pembeni imeibuka.

 

Video ya TikTok iliyoshirikiwa na Fantôme noir inaonyesha Mchungaji akihutubia mkutano wake akilaani vitendo kupigana na vifaranga wa pembeni.

 

“Sasa tukiua mpango kando vile mnataka, tuuwe wote tutabaki na nani na bwana yako ndio taka taka, mlafi.”

 

“Bwanako ndio mkulaji, ana kunywa coca ccola, kila soda akiona anataka kukula tuta ua wanawake wote juu ya hii kisirani moja?”

 

“Si tuue hiyo bwana yako mpango wa kando wabaki na watoto wao.”

 

“Usifikirie ni malaika, ni mtu tuu sasa anahitaji msaada wako umsaidie wakati ameingi ujinga , ukiona bwana yako ana aujinga umsaidie.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!