Home » Wanandoa 12 Nyandarua Wafunga Pingu Za Maisha

Furaha na shangwe zimeshuhudiwa katika kanisa katoliki la St. Teresa Equator huko Ol-Joro Orok Kaunti ya Nyandarua, ambapo maharusi 12 wamefanya harusi kwa wakati mmoja.

 

Wanandoa hao wamebadilishana viapo kanisani katika hafla ya kupendeza iliyohudhuriwa na mamia ya waumini na viongozi wa eneo hilo, akiwemo Mbunge wa Ol-Joro Orok Michael Muchir.

 

Askofu Joseph Mbatia wa Jimbo Katoliki la Nyahururu ameongoza ibada hiyo, ambapo imekua hafla ya kwanza katika eneo hilo.

 

Askofu Mbatia aliwakumbusha wanandoa wajibu wao katika kudumisha ndoa imara na yenye manufaa katika mahubiri yake.

 

Kulingana na Mbatia ubinafsi na ukosefu wa upendo wa kweli ni sababu kuu za migogoro katika familia nyingi, na kwamba hii huwafanya wengine kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa.
Makasisi waliwatia moyo waume na wake kufufua ndoa zao na kusitawisha upendo miongoni mwa washiriki wote wa familia.

 

Wanandoa waliohojiwa walieleza furaha yao kwa kutimiza ndoto zao za kufunga ndoa kwa mara ya kwanza, licha ya kwamba gharama kubwa ya kupanga iliwazuia kufanya hivyo peke yao.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!