Home » Ruto Atangaza Kukatwa Kwa Lazima Mishahara Ya Wafanyakazi Wote Wa Serikali

Ruto Atangaza Kukatwa Kwa Lazima Mishahara Ya Wafanyakazi Wote Wa Serikali

Rais William Ruto, ametangaza kwamba watumishi wote wa umma watakatwa asilimia 3 ya mishahara yao.
Rais Ruto, akihudhuria ibada katika Kanisa la Friends Church (Quakers) huko Donholm, Nairobi, amesema kuwa makato hayo yatasaidia Wakenya kupata nyumba za bei nafuu.

 

Kuhusu kwa nini watumishi wa umma watalazimika kutoa michango hiyo, Ruto ameeleza, Ili kuweze kuunda hazina ambayo itasaidia watu wa Kenya kupata nyumba bora lazima watumishi wa umaa wachangie.

 

Serikali ya rais Ruto inalenga zaidi kujenga nyumba elfu mia 200,000 za bei nafuu kufikia 2027 ili kunufaisha jamii milioni 2-3.

 

Rais ametangaza kwamba serikali tayari ilikuwa imejenga nyumba elfu 30,000 za bei nafuu jijini Nairobi.

 

Kama ilivyopendekezwa na Hazina ya Makazi, Ruto alifichua kuwa waajiri pia walipewa jukumu la kuchangia asilimia 6 ya mshahara wa wafanyikazi wao kwa kitita cha NSSF.

 

Rais alitangaza kwamba kila wakati serikali inapokopa kutoka kwa mfuko wa NSSF, italipa kwa riba, na kukuza mfuko huo zaidi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!