Bei za Unga: Linturi Aita Zaidi Ya Wasaga Unga 20 Na Kutishia Kufuta Vibali
Waziri wa Kilimo Mithika Linturi sasa anasema kwamba amewaita zaidi ya wasaga mahindi 20 wa humu nchini siku ya Ijumaa ili kujua ni kwa nini bado hawajapunguza bei ya unga.
Aidha Hii ni baada ya ukaguzi wa moja kwa moja wa wakenya kufichua kuwa ni mfanyabiashara mmoja pekee wa kusaga mahindi, aliyekuwa akiuza bidhaa zake chini ya shilingi mia 170 licha ya Rais William Ruto kutangaza hadharani kwamba gharama ya bidhaa hiyo ya kimsingi itapungua kwa kiasi kikubwa wiki hii.
Akizungumza na wanahabari,Linturi amebainisha kuwa ni muuzaji wa unga mmoja pekee aliyefuata masharti ya rais ruto kuhusiana na kupunguza bei ya bidhaa hiyo muhimu.
Waziri Linturi ameongeza kuwa wasagaji walioomba leseni lakini wamekaidi maagizo ya serikali wanahatarisha kunyang’anywa leseni zao.