Home » Mawaziri Kipchumba Murkomen Na Soipan Tuya Kufika Mbele Ya Bunge Leo Alasiri

Mawaziri Kipchumba Murkomen Na Soipan Tuya Kufika Mbele Ya Bunge Leo Alasiri

Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen na mwenzake wa Mazingira Soipan Tuya watakuwa kundi la pili la mawaziri kufika mbele ya kikao cha Bunge la Kitaifa leo hii Jumatano alasiri.

 

Wawili hao wanatarajiwa kujibu maswali yaliyoulizwa na wabunge yanayogusa wizara zao.

 

Waziri Murkomen atakuwa akijibu, miongoni mwa mengine, swali la Mwakilishi wa Wanawake wa Machakos Joyce Kamene kuhusu ukarabati wa daraja katika kivuko cha Hilton Garden Inn.

 

Pia ameratibiwa kujibu swali la Mbunge wa Rongo Paul Abuor kuhusu kuchelewa kukamilika kwa Barabara ya Riosiri-Rongo-Cham Gi Wadu.

 

Murkomen pia anatarajiwa kumjibu Mbunge wa Mwingi ya Kati Gideon Mulyungi kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa Barabara ya Kalisasi-Mumbuni, Awamu ya I na Awamu ya Pili.

 

Mulyungi pia alitaka majibu kuhusu kukwama kwa ujenzi wa Barabara ya Nguni-Nuu na Daraja la Enziu kaunti ya Kitui, pamoja na kukwama kwa ujenzi wa Barabara ya Mwingi-Slaughter House.

 

Mbunge huyo pia atataka kujua kutoka kwa waziri kuhusu mikakati ambayo wizara yake imeweka kuhusu kupunguza msongamano wa magari jijini tangu Barabara ya Nairobi Expressway kuanza kufanya kazi.

 

Naye……Waziri Tuya anatazamiwa kujibu maswala ya Mbunge wa Elgeyo Marakwet Caroline Ngelechei kuhusu kupungua kwa misitu licha ya marufuku ya kulima mahindi katika misitu.

 

Mbunge huyo ana wasiwasi kwamba eneo la msitu linakwenda chini katika Miradi ya Uanzishaji wa Mimea na Uboreshaji wa Maisha (PELIS).

 

Tuya pia atakuwa akijibu swali la Mbunge wa Mandera Kusini Abdul Haro kuhusiana na athari za mawimbi ya joto nchini.

 

Alhamisi iliyopita, kiongozi wa Wengi Bungeni Kimani Ichung’wah alisema mawaziri walioratibiwa kufika kwa vikao vya maswali watazinduliwa wiki moja kabla.

 

Jumatano iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki ndiye aliyekuwa wa kwanza huku wabunge wakimkabili kwa maswali mengi.

 

Wasiwasi kuhusu ukosefu wa usalama katika maeneo mbalimbali ya nchi, zaidi katika eneo la kaskazini mwa bonde la ufa, na jinsi polisi wanavyozima maandamano ulijitokeza katika mijadala hiyo.

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!