Home » Gachagua Ajibu Barua ya Raila ICC, Atoa Maelekezo kwa IG Koome

Gachagua Ajibu Barua ya Raila ICC, Atoa Maelekezo kwa IG Koome

Naibu Rais Rigathi Gachagua amepuuza barua ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), akiishutumu serikali kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano.

 

Kulingana na Gachagua ambaye alihutubia mkutano wa kisiasa katika Kaunti ya Nyandarua, Raila, na timu yake wanapaswa kutumwa Hague baada ya kuharibu mali za wakenya.
Gachagua alipinga, akithubutu Raila kuandamana baada ya Ramadhan, kama alivyotishiwa.

 

Gachagua aidha amemwagiza Inspekta Jenerali wa Polisi, Japhet Koome, kuendelea kutekeleza majukumu yake bila uoga wowote.

 

Amekariri kuwa serikali haitashurutishwa, Raila akithubutu kurejea barabarani mradi tu wasiharibu mali ya watu wengine.
Katika barua hiyo, wakili wa raila odinga Paul Mwangi alitoa madai 9 kwa ICC akiitaka mahakama hiyo kuchunguza hali ya kisiasa nchini Kenya.

 

Moja ya masuala ambayo mahakama ya kimataifa iliombwa kuchunguza ni Gachagua ambaye alishtakiwa kwa kuwanyima uhalali wanachama wa Azimio.

 

Azimio pia ilimshutumu Inspekta jenerali kwa kuunda kitengo cha polisi cha wahuni kuwalenga wafuasi wake wakati wa maandamano.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!