Home » Wahudumu Wa Afya Katika Kaunti 12 Hawataripoti Kazini Wiki Ijayo

Wahudumu Wa Afya Katika Kaunti 12 Hawataripoti Kazini Wiki Ijayo

Madaktari katika kaunti 12 sasa wanasema kuwa watasitisha huduma zao kuwa umma kuanzia Jumatano, Aprili 19, 2023 kutokana na kucheleweshwa kwa mishahara.

 

Kaunti zitakazoathirika ni; Kisumu, Mombasa, Nyamira, Kisii, Murang’a, Nyeri, Laikipia, Bomet, Nyandarua, Embu, Vihiga na Taita Taveta.
Katika taarifa ya pamoja kwa vyumba vya habari, wakuu wa Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini (KMPDU), Chama cha Kitaifa cha Wauguzi (K.NUN) na Muungano wa Maafisa wa Kliniki (K.U.C.O) wamesema kuwa wanachama wao bado hawajapokea malipo yao ya Machi, wakidai kuwa kuwaacha katika hali mbaya ya kifedha.

 

Wakuu wa Muungano wa Kitaifa wa Wataalamu wa Dawa nchini Kenya na Jumuiya ya Wataalamu wa Afya ya Kenya pia wameunga mkono kauli hiyo.

 

Aidha wakuu hao wa miungano wamezitaka kaunti zitakazoathiriwa na hatua hiyo kushughulikia malalamishi yao kwa dharura ili kuepusha kutatizika zaidi kwa huduma za kiafya.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!