Home » Mtoto Mmoja Afariki Na Wengine 9 Kujeruhiwa Katika Ajali Ya Barabara Ya Makueni

Mtoto Mmoja Afariki Na Wengine 9 Kujeruhiwa Katika Ajali Ya Barabara Ya Makueni

Mtoto mmoja alifariki na wengine kumi kujeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea eneo la Kiangi kwenye barabara ya Wote – Makindu leo asubuhi.
Watoto hao walisemekana kuwa walikuwa wakielekea shuleni wakati basi walimokuwa wakisafiria kufeli breki na kuanguka.

 

Mwanafunzi wa PP1 mwenye umri wa miaka mitano aliaga dunia papo hapo, huku wengine 10 wakikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Makueni kwa matibabu.

 

Kwa mujibu wa walioshuhudia ajali hiyo inadaiwa kuwa basi hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva asiye na leseni ambaye pia alijeruhiwa wakati wa ajali hiyo.

 

Dkt Joseph Masila, afisa msimamizi katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Makueni, amesema waliojeruhiwa kwa sasa wanaendelea kupata nafuu na hali zao zinaendelea vizuri.

 

Mwili wa mwanafunzi aliyepoteza maisha ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha kituo hicho huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!