Home » Kenya Kwanza Wazindua Wajumbe Saba Watakaoongoza Mazungumzo Na wenzao Wa Azimio

Kenya Kwanza Wazindua Wajumbe Saba Watakaoongoza Mazungumzo Na wenzao Wa Azimio

Muungano wa Kenya Kwanza umezindua wajumbe wake saba ambao wataungana na wenzao wa Azimio katika mazungumzo ya bunge la pande mbili.

 

Wakati wa kikao na wanahabari katika Ikulu leo hii Jumanne, Kiongozi wa wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah amesema kuwa wabunge hao walichaguliwa kufuatia majadiliano wakati wa mkutano wa awali wa Kikundi cha Wabunge wa Kenya Kwanza.

 

Seneta wa Kakamega Boni Khalwale, wa Bomet Hillary Sigei, Seneta Mteule Essy Okenyuri, Mwakilishi wa Wanawake wa Taita Taveta Lydia Haika, Mbunge wa Tharaka George Murugara, Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse, na wa Edlas Adan Keynan ni miongoni wale waliogaliwa na Kenya kwanza.

 

Kulingana na Ichung’wah, walikubaliana na Rais William Ruto kuhusu umuhimu wa kutawala nchi kwa mujibu wa sheria na kushirikiana na upinzani kwa ajili ya nchi.

 

Muungano wa Azimio la Umoja, kwa upande wao, ulizindua timu ya watu saba mnamo Alhamisi, Aprili 6, wakati wa mkutano wa Kikundi cha Wabunge huko Machakos.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!