Home » Watu 3 Wakamatwa Kwa Mauaji Ya Kasisi Wa Mt Elgon

Polisi katika kaunti ya Bungoma wamewatia mbaroni washukiwa watatu kufuatia mauaji ya mchungaji mmoja mnamo Aprili 7 huko Kaptama, Mlima Elgon.

 

Wapelelezi kutoka idara ya Upelelezi na makosa ya Jinai DCI leo hii Jumanne wamewataja watatu hao kuwa Job Mosobin almaarufu Malilo, Geoffrey Kimutai almaarufu Kus Kus na Andrew Ngeiwa almaarufu Michuki.

 

Kukamatwa kwao kunajiri baada ya maafisa wa polisi kushirikiana na wananchi katika msako wao.

 

Watatu hao wanasemekana kumkabili Mchungaji David Ngeiwa alipofunga duka lake mwendo wa saa tatu usiku huo wakiwa na bunduki aina ya AK-47 na kuondoka na kiasi cha pesa kisichojulikana.

 

Mchungaji huyo alifariki dunia wakati akipewa matibabu katika kituo cha matibabu cha Sikotia.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!