Home » Rosa Ree Adai Maisha Yamekuwa Magumu Kikazi

Rapa kutoka Tanzania na Exgirlfriend wa Timmy Tdat, Rosa Ree ameeleza kuwa hafanyi vizuri kimuziki kupitia posti ya Instagram.

 

Mwanamuziki huyo alichapisha video yake akilia akisema hayuko sawa. Rosa Ree alisema angetaka kushiriki lakini wanablogu na vyombo vya habari vingechukua story na kusahau kuhusu maumivu yake.

 

“Siko sawa! Naumia! Ninapitia hali ngumu! Ninachoona ni giza tu. Najiuliza maswali bila majibu.”

 

Rapa huyo alieleza kuwa alijihisi yuko pekee yake na hata watu anaowatumbuiza hawapo wakati yeye anawahitaji.

 

“Nikiwa hivi nakimbilia kwa nani? Umekuwa ukiburudika na mimi lakini nisipokuwa sawa utanisaidia? Naweza kujitokeza na kuwa muwazi kwa chochote ninachopitia lakini najua baadhi. mtanicheka, kusengenya, kujitenga na wengine hata hawajali.”

 

Aliendelea kueleza kwamba uchungu wake ungetumiwa kuwaburudisha wasengenyaji na maisha yangeendelea kwa kila mtu mwingine hata ikiwa ameenda.

 

“Nikiongelea haya ninayopitia itakuwa vichwa vya habari kwenye blogu za udaku, nitapokea simu za kufanya mahojiano ili media house wapate story, maisha yangu ni movie tu ili watu wapate views. hisia zangu? Hata nisipoishi, maisha bado yataendelea sawa…kusema kweli, siko sawa.”

 

Uongozi wa Rosa Ree umetoa taarifa ukionyesha kuwa kwa sasa rapper huyo yuko na familia yake na ameomba faragha wakati huu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!