Home » Mbunge Kiunjuri Ataka Ushirikishwaji Katika Mazungumzo Ya Ruto-Raila

Mbunge Kiunjuri Ataka Ushirikishwaji Katika Mazungumzo Ya Ruto-Raila

Kiongozi wa Chama cha TSP Mwangi Kiunjuri ametaka kamati shirikishi itakayoundwa kuchunguza madai yaliyotolewa na kundi la Azimio badala ya suala hilo kuchukuliwa na Wabunge pekee.

 

Aidha, Kiunjuri ameitaka kamati hiyo pia kuangalia jinsi katiba inavyofaa kufanyiwa marekebisho ili kuleta usawa nchini.

 

Mbunge huyo wa Laikipia Mashariki amesema kuwa zaidi ya watu milioni saba hawakuwahi kushiriki uchaguzi wa mwaka jana na maoni yao yanahitaji kusikilizwa akihoji kwa nini viongozi kutoka nje ya Bunge hawawezi kujumuishwa katika kamati hiyo.

 

Ametoa wito wa kujumuishwa kwa viongozi wa kidini na wataalamu wengine akiongeza kuwa matatizo ya Wakenya yanahitaji suluhu za Wakenya.

 

Vile vile Amebainisha kuwa wakati wa kupitishwa kwa katiba rais na viongozi wa kanisa walipinga huku Rais wa zamani Uhuru Kenyatta na kiongozi wa Upinzani wakiunga mkono jambo ambalo kwa sasa ni kinyume.

 

Kuhusu uwakilishi amesema baadhi ya kaunti zina uwakilishi zaidi huku zingine zikihangaika linapokuja suala la kugawana rasilimali na hili linapaswa kushughulikiwa kwa wakati huu.

 

Amekuwa akizungumza alipokuwa akitoa ufadhili wa zaidi ya Ksh milioni 50 kwa ajili ya masomo kwa wanafunzi katika Eneobunge lake la Laikipia Mashariki.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!