Home » Raila Azindua Washirika 7 Watakaoshiriki Mazungumzo Na Serikali

Raila Azindua Washirika 7 Watakaoshiriki Mazungumzo Na Serikali

Seneta wa Narok Ledama Ole Kina na mwenzake wa Nairobi Edwin Sifuna ni miongoni mwa timu ya wabunge saba waliochaguliwa na Azimio la Umoja one-kenya leo hii Alhamisi, kuwakilisha mrengo huo katika shughuli zilizoratibiwa za bunge la pande mbili.

 

Katika orodha hiyo iliyotumwa na katibu wa masuala ya kisiasa wa chama cha Kanu, Fredrick Okango, Seneta wa Kitui Enoch Wambua pia alikuwa miongoni mwa viongozi waliochaguliwa na Raila.

 

Wengine wanne wametoka Bunge la Kitaifa, akiwemo Amina Mnyanzi wa (Malindi), Millie Odhiambo wa (Suba Kaskazini), David Pkosing wa (Pokot Kusini) na Otiende Amollo wa (Rarieda).

 

Kikosi cha Raila cha watu saba kimechaguliwa wakati wa mkutano wa wabunge wa Azimio la Umoja katika Kaunti ya Machakos.

 

Kiongozi huyo wa ODM ameongoza mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na uongozi mkuu wa muungano huo akiwemo kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua.

 

Azimio imechagua viongozi saba kufuatia makubaliano ya mrengo huo kusitisha maandamano na kushirikiana na upande wa serikali katika masuala manne waliyoibua.

 

Ikumbukwe kwamba upande wa Rais William Ruto wa Kenya Kwanza bado haujatoa orodha yake ya wabunge watakaozungumza na Azimio.
Katika mkutano huo, mrengo unaoongozwa na Raila umekariri haja ya timu hiyo kuongezwa nje ya bunge huku wakishikilia kuwa hawana nia ya kushiriki serikali.

 

Rais Ruto kwa upande wake alisisitiza kuwa masuala hayo yatashughulikiwa tu bungeni kwani wana mamlaka ya kurekebisha sheria.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!