Home » Raila Aidhinisha Kutupwa kwa Sabina Chege Kama Kinara Wa Wachache Wa Azimio

Raila Aidhinisha Kutupwa kwa Sabina Chege Kama Kinara Wa Wachache Wa Azimio

Muungano wa Azimio la Umoja umemfukuza Mbunge mteule Sabina Chege kama Kinara wake wa Wachache katika Bunge la Kitaifa.

 

Akizungumza na wanahabari, afisa wa chama cha KANU Frederick Okang’o amebainisha kuwa uamuzi huo ulifikiwa wakati wa Mkutano wa Kundi la Wabunge wa Azimio la Umoja ambao ulifanyika katika Kaunti ya Machakos leo hii.

 

Kushushwa cheo kwa Sabina kumejiri saa chache baada ya Kiongozi wa Chama cha (ODM) Raila Odinga kupendekeza mabadiliko ya sheria ili kuwaadhibu viongozi waliokaidi masharti ya Azimio.

 

Sabina alikuwa amekashifiwa kwa muda mrefu kwa kutangaza kuunga mkono utawala wa Kenya Kwanza wakati wa ziara yake katika Ikulu mnamo Januari 28, 2023.

 

Katika mkutano huo, Sabina alitoa wito kwa wananchi kumuunga mkono Rais William Ruto na Naibu Rais Rigathi Gachagua kama Mfalme wa Mlima Kenya.

 

Mbunge huyo mteule alikubaliana na Rais Ruto na Naibu wake kuhusu miradi kadhaa ambayo ilianzishwa na utawala uliopita.

 

 

Hata hivyo, alipokuwa akihutubia Azimio la Umoja , Raila aliwashutumu wabunge waliomuunga Rais Ruto mkono akisema wao ni wasaliti wa kisiasa.

 

Katika mapendekezo ya Kamati ya Vyama viwili, Raila alibainisha kuwa sheria inafaa kubadilishwa ili kuruhusu vyama vya kisiasa kuwaadhibu wanachama walaghai.

 

Raila anataka mamlaka kuchukua nafasi ya wabunge walioteuliwa ambao walivuka mipaka ya vyama ili kuunga mkono muungano au chama kingine cha kisiasa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!